Burudani

Nakaaya awalaumu Fid Q na Klynn

Nakaaya awalaumu Fid Q na Klynn
Inasemekana kwamba mwanadada Nakaaya amekerwa sana na kitendo cha
wasanii wawili kutomuonesha ushirikiano katika kazi. Habari zinasemea
kuwa Nakaaya aliwaomba wasanii wengi wakali wajitokeze studio wakati wa
kurecord wimbo wake wa ‘I am an African’ na kuingiza sauti zao katika
ngoma hiyo, lakini Fid Q na K-Lyinn walishindwa kutokea

Wimbo umekamilika bila ya sauti zao na video pia ipo tayari, waliyoshirikishwa katika ngoma hiyo ni Chidi Beenz, Lufunyo na wengine.

Kwa upande mwingine Fid Q aliteta na DJ Fetty wa Clouds FM na kumuambia "Nakaaya alinipigia simu mida ya mchana na kuniambia niende studio saa hiyo, ndio nikamwambia angeniambia mapema maana nilikua mjini na mihangaiko mingine na nisingeweza kufika studio saa hiyo hiyo aliyonipigia simu. Unajua Fetty mi hayo mambo nilishaacha zamani nikajirekebisha nisengependa kurudi huko. Hata kama ni wewe Fetty mtu anakupigia simu saa hiyo hiyo anataka uende studio hautaweza kweli kwasababu tayari unakuwa na mipango yako kichwani. Angeniambia kabla ningeenda, kwanini nikatae?!".

Kama hayo ni kweli, hatuoni sababu ya kujenga chuki kwa vile ni mambo ambayo yanatokea…wasanii wetu waendelee kufanya kazi kwa moyo mmoja.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents