Nako2Nako wanajipanga

Nako 2 Nako, DJ Fetty na Joh Makini

Nako 2 Nako, DJ Fetty na Joh Makini

Wakali wanaowakilisha pande za Arusha katika game la Bongo Flava, Nako
2 Nako wamesema sasa ni wakati wa mambo mapya na wameingia ndani ya
studio ya B-Hitz kujipanga kwamakamuzi kama nyuki mwanzo mwisho.

Baada ya kila mmoja kutoka kivyake Nako 2 Nako wanatarajiwa kurudi mtamboni wakiwa kama kundi kamili kasoro Ibra Da Hustler aliyejitoa.

“Unajuwa tulikuwa kimya muda mrefu kwasababu member wa kundi kila mmoja
alikuwa anafanya kazi kama solo, wote tumeshamaliza na sasa tumerudi
kama zamani, yani mikandamizo inaendelea mwanzo mwisho, walisema mengi
kuwa tumevunjika, tumesambaratika lakini sasa ni wakati wa kuwapa mambo
matamu na mazuri” alisema Lordeyes.

Haya sasa wapenzi na washabiki wa Nako 2 Nako jamaa ndio hao
mtamboni wameshaanza kurekodi nyimbo kwahiyo ni wakati wa mkao wakula
tu sasa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents