Burudani

Nakubali anachofanya Alikiba – Q Boy Msafi

Msanii wa muziki Bongo na mbunifu wa mavazi, Q Boy Msafi amesema anakubali kile anachofanya Alikiba katika muziki.

Akizungumza na Bongo5 muimbaji huyo amesema Alikiba anafanya vizuri katika muziki ila kwa upande wa mavazi kuna kitu ambacho kimepungua.

“Na appriciate anachokifanya na naweza kusema ni miongoni mwa watu ambao naona kuna gap fulani katika uvaaji wake, nikipata ile nafasi naweza kufanya kitu ambacho upeo wangu niliokuwa nao kwamba kuna kitu hiki na hiki naweza kukiweka hapa kikapatikana kitu ambacho kikaleta utofauti,” amesema.

Ameongeza kuwa hamaanishi wanaohusika na mavazi ya Alikiba wanafanya vibaya ila kuna mabadiliko fulani anaweza kufanya katika mavazi yake. Q Boy Msafi aliwahi kuwa mbunifu wa mavazi ya Diamond Platnumz.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents