Habari

Nakumatt kuzinunua supermarket tatu za Shoprite Tanzania

Wamiliki wa supermarkert za Nakumatt za nchini Kenya wapo kwenye maongezi na wamiliki wa maduka ya Shoprite wa Afrika Kusini kununua maduka matatu ya Shoprite ya nchini Tanzania katika nia yake ya kujipanua zaidi.

page

Mkurugenzi Mtendaji wa Nakumatt, Atul Shah alisema kampuni hiyo inataka kuzichukua supermarket hizo za Shoprite, ambapo mbili zipo Dar es Salaam na moja jijini Arusha. Kampuni hiyo yenya maduka nchini Kenya, Uganda na Rwanda, tayari inayo supermarket yake mjini Moshi.

Hata hivyo Shah hakuweka wazi thamani ya manunuzi hayo yanayotaliwa kukukamilika miezi mitatu hadi mitano ijayo lakini akasema itawezeshwa kupitia mikopo kutoka kwa taasisi zinazoikopesha kampuni hiyo.

Source: Reuters via ThePost (SA)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents