Burudani

Nameless wa Kenya kuja na album mpya 2014 ‘Kabla Hajastaafu’

Ni muda mrefu umepita bila kusikia kitu kipya kutoka kwa nyota wa +254 Nameless ambaye pia ni mume wa msanii mwingine maarufu wa Kenya Wahu.

nameless

Nameless aliyewahi kuhit bongo na single zake ‘Sinzia’ na ‘Salary’ ana mipango mizuri ya kuuvunja ukimya huo mwaka huu (2014) ambapo anategemea kutoa album yake mpya aliyoipa jina la ‘Before IR’ yaani kwa kirefu ‘Before I Retire’ (kabla sijastaafu).

Kwa mujibu wa NIAJE ya Kenya, album hiyo itabeba nyimbo 20 na Nameless amedai kuwa itauonesha upande wa pili wa msanii huyo ambao watu hawaujui.

David Mathenge aka Nameless ni baba wa watoto wawili (Tumiso na Nyakio) aliowapata na mke wake Wahu Kagwi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents