Afya

Namna ya kuepuka kutoa harufu mbaya miguu

Miguu kutoa harufu mbaya ni tatizo ambalo linawakabili baadhi ya watu katika jamii hususani wanaume.

Kuna njia zipo ambayo zinaweza kuwa msaada kwako kwa wewe mwenye tatizo hili.

1. Endapo umegundua unatatizo la kunuka miguu basi hakikisha unasafisha miguu yako mara kwa mara na kuikausha vizuri ili kuepusha unyevunyevu.

2. Kila unapovaa viatu vya kufunika hakikisha unavaa soksi zilizo safi na kavu.

3.Nikosa kurudia soksi zilizo valima zaidi ya mara moja bila ya kufua au ambazo hazijakauka vizuri kwani huweza kuchangia miguu kunuka zaidi.

4. Usivae viatu vilivyo vibichi au vilivyoloa na endapo ikatokea umenyeshewa, hakikisha unavianika kwenye hewa ili vikauke ili kupunguza uwezekano wa kutoa harufu.

Licha ya uwepo kwa sababu tofauti tofauti zinazochangia tatizo la kunuka miguu, ukweli ni kwamba uchafu ndio chanzo kikuu cha miguu kutoa harufu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents