Burudani

Nampenda Diamond kwa sababu ni mnyenyekevu, simpendi Alikiba ni kiburi – Mch. Anthony Lusekelo

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu kwa jina la Mzee wa Upako, amemtaja msanii ambaye anamkubali kati ya Alikiba na Diamond pamoja na kutoa sababu zake.

Akiongea na kipindi cha Maisha Mseto cha Times FM, Mzee huyo wa Upako amesema anampenda sana Diamond kwa sababu ni mnyenyekevu lakini Alikiba ni kiburi.

“Mimi nampenda sana Diamond kwa sababu ni mnyenyekevu, Simpendi Alikiba kwa sababu ana kiburi, nadhani kwa sababu amekaa Kariakoo,” amesema Lusekelo.

Mchungaji huyo ameongeza kwa kusema, “Ukipigia simu Diamond anapokea kwa unyenyekevu ila Alikiba anapokea kwa maringo. Ndio maana Diamond amefika mbali.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents