Michezo

Nampiga Man United nyumbani kwangu – Jurgen Klopp

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesisitiza wachezaji wake Philippe Coutinho na Roberto Firmino watakuwepo katika mchezo wake dhidi ya Manchester United.

Wachezaji ni wakimataifa wa Brazili ambao walikuwa katika majukumu ya kutumikia timu yao ya taifa katika kuhakikisha wanapata nafasi ya kushiriki kombe la dunia mwakani nchini Urusi.

Hatahivyo, Klopp amesema wachezaji wote wawili watakuwa katika mchezo huo ambapo Coutinho ataziba pengo la Sadio Mane ambaye ni majeruhi.

“Phil amecheza michezo miwili tu wakati Roberto akiwa amecheza kama dakika tano hivi hivyo naamini nitofauti bilashaka lakini hawa wote itabidi wacheze na watakuwa sawa na uwepo wao ni muhimu,” amesema Meneja huyo wa Liverpool.

Kwa upande wa United, ambayo inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi ya Uingereza ikiwa ni tofauti ya magoli dhidi ya Man City watahitaji ushindi ilikujihakikishia wanakuwa kileleni mwa msimamo.

Ingawa wapo ugenini Anfield, Jose Mourinho amesema ” Nafikiri watu wakizungumzia hali ya ushindani utakao kuwepo katika mchezo huo wanadhani hatupendi la hasha.”

“Hivi ndivyo tunavyohitaji nashitushwa na namna mnavyozungumzia vibaya kwa sisi kwenda Anfield tena hadi wachezaji wakubwa wazamani, hatuhofii inatuongezea hamasa na ndivyotunavyopenda kitu ambacho tungependa kiwepo katika kila mchezo.”

Habari kutoka katika klabu zote mbili ni kwamba, Mane hatokuwepo kwa kipindi cha wiki sita na nafasi yake itazibwa na Coutinho huku  Emre Can akicheza nafasi ya kiungo.

Adam Lallana anaendelea kupata nafuu na atarejea hivi punde.

Marouane Fellaini hatakuwepo katika mchezo huo kutokana na majeraha aliyoyapata wakati akiitumikia timu yake ya taifa ya Ubeligiji na kuungana na kiungo Michael Carrick and Paul Pogba.

Marcos Rojo na Zlatan Ibrahimovic wanaendelea kuwa fiti baada ya kutoka katika majeraha waliyokuwa wameyapata lakini Mourinho ameonyesha kuwa wachezaji Phil Jones na Romelu Lukaku watakuwepo.

Takwimu za timu hizi mbili Liverpool dhidi ya Manchester United

Liverpool imekuwa ikiutafuta ushindi katika michezo ya Ligi Kuu nchini Uingereza dhidi ya Manchester United na kuambulia suluhu mbili na kupoteza michezo minne (D2 L4),hii ikiwa ni kwa michezo nane ya tangu mwaka 2004 na 2008.

Katika mashindano yote Liverpool dhidi ya Manchester United imeshinda mchezo mmoja kati ya michezo saba ikitoa suluhu mitatu na kupoteza minne (W1 D3 L4) ambapo ushindi huo ilikuwa wa jumla ya mabao 2-0 michuano ya Europa League mwaka 2015/16.

Jurgen Klopp amepoteza mmoja tu kati ya michezo yote dhidi ya  Jose Mourinho (W3 D3 L1).

Jose Mourinho akishinda michezo nane kati ya 10 ya ligi ya Uingereza  akikutana na Liverpool (D1 L1) kati ya Octoba mwaka 2004 na Novemba mwaka 2014.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents