Burudani

Namshukuru sana Alikiba kwa kuimba wimbo wa kunitukuza – Yvonne Chakachaka

Msanii mkongwe wa muziki kutoka Afrika Kusini, Yvonne Chakachaka amesema amemmwagia sifa muimbaji wa ‘Mvumo wa Radi’ Alikiba kwa madai ni msanii mwenye kipaji cha hali ya juu.

Akiongea na Clouds FM, Jumatano hii Chakachaka amesema wimbo huo ambao amefanya AliKiba ni wimbo ambao unawatetea akina mama.

“Mimi na Ali tumeandika wimbo pamoja, una vibe ya “Mkomboti” na tumeimba kwa Kiswahili. Ali yupo comfortable sana kuimba kwenye kiswahili na alinifundisha kiasi kidogo cha Kiswahili,”

Aliongeza, “Wimbo wenyewe unawatukuza wanawake, akina Mama – Ali anaonekana ni kijana mzuri sana na namshukuru sana kwa kuimba wimbo wa kunitukuza mimi kama Mama na wanawake wengine Afrika.”

Chakachaka yupo nchini Tanzania kwaajili ya shughuli za kijamii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents