Namungo FC wapewa onyo kali kosa wachezaji kuvaa jezi namba zaidi ya 60

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Septemba 15, 2020 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi yafuatao;

Mechi namba 1: Namungo FC 1-0 Coastal Union FC

Timu ya Namungo FC imepewa onyo kali kwa kosa la kuchezesha wachezaji wakiwa wamevaa jezi zenye namba zaidi ya sitini (60) katika mchezo tajwa hapo juu uliochezwa Septemba 6, 2020 katika uwanja wa Majaliwa.

Namungo FC ilichezesha wachezaji wawili waliovaa jezi zenye namba zaidi ya sitini (60), wachezaji hao ni Haruna Shamte aliyevalia jezi namba 88 na Shiza Ramadhani Kichuya aliyevalia jezi namba 77. Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 15(2.5)-15(54) kuhusu taratibu za mchezo.

Hali kadhalika timu ya Coastal Union FC imepewa onyo kali kwa kosa la kuchelewa kufika uwanjani kwa muda muafaka katika mechi hiyo. Coastal Union ilifika uwanjani saa saba 7:06 mchana badala ya saa 6:30 mchana.
Pia kamishna wa mchezo wa Namungo FC dhidi ya Coastal Union FC Bw.

Juma Mpuya amekumbushwa kusimamia majukumu yake kikamilifu kufuatia tukio la kuruhusu wachezaji wa Namungo FC kucheza mechi hiyo huku wakiwa wamevaa jezi zenye namba zaidi ya sitini (60) hali ilyosababisha uvunjifu wa kanuni namba 15 ya taratibu za mchezo.

Mechi namba 12: JKT Tanzania FC 0-2 Dodoma Jiji FC

Timu ya JKT Tanzania imepewa onyo kali na kutakiwa kujali muda sanjari na taratibu za michezo ya Ligi wakati wote baada ya kusababisha kuchelewa kuanza kwa mchezo wao dhidi ya Dodoma FC kwa dakika 15 na hivyo kupelekea uanze saa 8:15 mchana kutokana na timu hiyo (mwenyeji) kutoleta gari ya kubeba wagonjwa (Ambulance) kwa wakati lakini baada ya dakika ya 15 gari ya wagonjwa ilifika uwanjani na mchezo ulianza na kumalizika kimalifu kwa dakika zote 90.Adhabu hii imetolewa kwa uzingativu wa kanuni ya 15(2.12)-(15:3(3) ya taratibu za mchezo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW