Burudani

Nando wa Tanzania arudi mjengoni kwa kishindo kwa kura za nchi 5, Betty wa Ethiopia na Motamma wa Botswana watolewa

Ukiwa umekamilika mzunguko wa wiki ya 4 katika mchezo wa ‘The Chase’ Afrika inashuhudia washiriki wengine wawili wakiuaga mchezo, Motamma wa Botswana na Betty wa Ethiopia ndio waliotolewa mchezoni katika eviction show ya jana Jumapili (June 23).

Betty
Betty

Motamma
Motamma

Zikiwa zimebaki siku 63 za kumjua mshiriki atakayeondoka na dola $300,000 za biggie tayari washiriki 8 wameshaliaga shindano na nyumba za Diamond na Ruby kubaki na washiriki 20.

Eviction ya Betty jana imemuachia upweke kipenzi chake Bolt ambaye hata hivyo wiki hii video nyingine ya wapenzi hao wakiwa kwenye ‘kwichi kwichi” (kwa sauti ya gossip cop Soudy Brown wa Clouds FM) mara ya pili ilivuja mtandaoni, huenda waliamua kuagana sababu wote walikuwa katika dangerzone.

Betty ndio mshiriki wa kwanza wa kike apple lake kung’atwa mjengoni na Bolt wa Sierra Leone kitu ambacho mama yake Betty amemtetea kwa kusema kuwa hizo zilikuwa ni ‘camera trick’ zilizofanywa na haters.

Eviction ya Betty imefanya Ethiopia ibaki na muwakilishi mmoja ambaye ni Bimp na Botswana ikiwa inawakilishwa na Oneal baada ya Motamma kutoka.

Nando wa Tanzania aliyekuwa miongoni mwa washiriki 7 waliokuwa nominated, ndiye mshiriki aliyeokolewa na kura za nchi 5 za Afrika zikiwemo Kenya na Uganda (sasa nguvu ya East Afrika inaonekana).

Oneal wa Botswana ndiye aliyefuatia kwa kupata kura za nchi 4, akifuatiwa na Natasha wa Malawi kwa kura za nchi 3.

Kutokana na kwamba Bolt, Elikem and Betty walipata kura ya nchi moja moja, ilitumika sheria ya kuangalia mwenye asilimia ndogo zaidi kati yao ambaye aliibuka kuwa Betty ndiye atoke. Cha kushangaza Botswana haikumpigia kura mshiriki wao mwingine Motamma na kumfanya kukosa hata kura moja ya nchi yake, na badala yake waliamua kukusanya nguvu zao kumpigia kura Oneil ambaye kweli amefanikiwa kubaki.

Hivi ndivyo kura zilivyopigwa kwa washiriki wote 7

votes

Angola: Oneal
Botswana: Oneal
Ghana: Elikem
Kenya: Nando
Ethiopia: Betty
Malawi: Natasha
Namibia: Nando
Nigeria: Nando
South Africa: Oneal
Sierra Leone: Bolt
Tanzania: Nando
Uganda: Nando
Zambia: Natasha
Zimbabwe: Natasha
Rest of Africa: Oneal

Total: Nando = 5; Oneal = 4; Natasha =3, Bolt = 1, Elikem = 1, Betty = 1, Motamma = 0. (Total: 15 Votes)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents