Soka saa 24!

Nandy adai alikuwa afunge ndoa na Ruge mwezi mmoja kabla ya kifo

Msanii wa muziki nchini, Faustina Charles Mfinanga maarufu kama Nandy rasmi amefunguka kuhusu mahusianao yake na marehemu Boss Ruge ambapo ilitarajiwa mwezi March mwaka huu wangefunga ndoa amabayo ingehudhuriwa na watu wengi wakubwa na maarufu hapa nchini na nje ya nchi pia.

Nandy akizungumza na AYO TV, amekiri kuwa na mahusiano mazito na Boss Ruge yaliyodumu kwa takribani miaka mitatu, na tayari wawili hao walikuwa wametambulishana na kukubalika kwa wazazi wa pande zote mbili.

Ametaja sababu ya kutoweka mahusiano yao mitandaoni na kusema kuwa hawakupenda mahusiano yao yaendeshwe na mitandao kwani walijua madhara makubwa yatokanayo na tabia ya kuweka mahusiano kwenye mitandao ambayo kwa kiasi kikubwa yangepelekea wawili hao kutotimiza mipango yao kimaisha.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW