Habari

‘Nang’atwa na nyuki 300 kila siku’-Ajutia kijana aliyeacha udaktari na kuuza nyuki

Waswahili wanasema acha kazi uone kazi kupata kazi. Huu msemo huenda ukaendana kabisa na maisha ya kijana Suk Mahammad Dalal ambaye inamlazimu kubeba nyuki na kupeleka kwa wataalamu wa kutengeneza dawa baridi.

Kijana Dalal (32) alikuwa Daktari Msaidizi katika chuo cha kutengeneza dawa baridi cha ISM mjini Kolkata nchini India ambapo aliamua kuacha kazi hiyo miaka 3 iliyopita kutokana na udogo wa mshahara aliyokuwa akilipwa.

Dalal anasema alipokuwa chuoni hapo aliona Madawa mengi yakitengenezwa kwa asali na nyuki huku akishuhudia wauzaji wa malighafi hizo wakiondoka na maburungutu ya pesa kitu ambacho kilimfanya avutiwe na biashara hiyo.

Hata hivyo, kwa maamuzi yake aliamua kuacha kazi na kukimbilia katika mji wa Chandramonipur, Jimbo la Bengal Magharibi mwa India ili kuanza kazi ya kulina asali na kuwakamata nyuki.

Dalal

Nilipokuwa mdogo kabla hata ya kujiunga na Chuo nilikuwa napenda kukwea miti hivyo uwezo huo ulinijengea imani kubwa kuwa biashara hiyo ningeiweza ingawaje nilijua fika kwamba nitang’atwa na nyuki.“amesema Dalal.

Bw. Dalal anasema alipofika huko alianza kuchonga mizinga ya kienyeji lakini soko la bidhaa hiyo halikuwa zuri hivyo ilikuwa inamlazimu kuvuna asali kwa njia ya kienyeji na kusafirisha nyuki kwa kutumia nguo kila siku.

Akielezea changamoto ya kusafirisha nyuki amesema ilikuwa inamlazimu kuweka nyuki hao kwenye fulana huku kila siku wakati akisubiri miezi minnne ya asali kutengenezwa na nyuki hao.

Anasema nyuki hao alikuwa anawahifadhi kwenye ndoo maalumu ambapo walikuwa kila wakijaa anawapeleka mjini Bengal kwa ajili ya mauzo.

Hata hivyo anasema biashara haikuwa nzuri kivile! kama ilivyokuwa awali kipindi akifanya kazi ya kutengeneza madawa.

Nilikuwa na matarajio makubwa ya biashara hii, lakini baada ya kuianza ghafla soko lake likaanza kudorora nusu nikate tamaa, lakini nikajikaza najua ipo siku mambo yatakaa sawa,“amesema Dalal.

Dalal amesema kutokana na uzoefu wa kukamata nyuki wa miaka 3, mwili wake umekuwa sugu kwani kila siku iendayo kwa mungu amedai anang’atwa na nyuki 300 na dawa yake kubwa anakunywa kikombe kimoja cha chai .

Nang’atwa na zaidi ya nyuki 300 kila siku, mwanzoni niliumia sana ila kwasasa naona kawaida siku wakining’ata wengi naenda kunywa kikombe kimoja cha chai kupunguza maumivu,“amesema Dalal.

Dalal anatumia mikono kuwashika nyuki hao bila kifaa chochote kila siku na kuwafunga kwenye fulana tayari kwa kuwahifadhi kwa ajili ya biashara. Tazama video ikimuonesha Dalal akiwa kwenye kazi yake


Chanzo:Daily Mail

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents