Nani Hizbu? CCM au CUF

Baada ya kujibu makombora ya chama tawala CCM, sasa Chama Cha Wananchi (CUF) kimebaini wazi kuwa hali imebadilika na kuonekana sasa vyama hivyo vinakitumia chama cha Hizbu ili kuchafuana

Baada ya kujibu makombora ya chama tawala CCM, sasa Chama Cha Wananchi (CUF) kimebaini wazi kuwa hali imebadilika na kuonekana sasa vyama hivyo vinakitumia chama cha Hizbu ili kuchafuana.


 


Mara tu hatua huyo kudhihiri, imebainika wazi kuendelea kuwepo kwa uhasama kati ya CCM na CUF hususani baada ya kurushiana madongo kisiasa na kupakana matope kwa kuwahusisha viongozi wa ngazi ya juu baina ya vyama hivyo viwili.


 


Ambapo CCM waliokuwa ni wa kwanza kuwatupia dongo CUF kwa kupitia kwa kada wake mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru kwamba chama hicho kina uhusiano wa moja kwa moja na chama hicho cha kisultani cha Hizbu na jana CUF wakajibu mapigo hayo kwamba CCM ndio wana historia ya kuwa na uhusiano na chama hicho cha Hizbu huku wakiwataja viongozi wa ngazi ya juu akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ally Hassan Mwinyi na mke wa Rais wa Zanzibar Bi Shadya Karume.


 


Wengine waliotajwa katika orodha hiyo ya uanachama wa Hizbu ni pamoja na Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansour Yusuf Himid ambaye ni ndugu wa mama Karume ambao wote ni wajukuu wa Sheikh Mohammed Salim Jinja ambaye ni mwanzilishi wa chama hicho cha Hizbu.


 


Achilia mbali viongozi hao, CUF walidai kuna kiongozi mwingine ambaye ni waziri katika Serikali ya Muungano kwamba aliwahi kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho cha Hizbu ambao ulikuwa ukijulikana kama Youth Own Union (YOU).


 


Kwa majibu hayo mkanganyiko umetanda miongoni mwa jamii kuhusu hasa ni nani kati ya pande zote mbili ambaye anahusika na chama hicho ama vyama hivyo vimeamua kutumia silaha hiyo kuchafuliana majina.


 


Suala hili liliwahi kuibuka ghafla siku chache kabla ya uchaguzi Mkuu uliopita baada ya gazeti moja la kila siku kutoa picha katika kurasa zake inayomuonesha aliyekuwa mgombea urais, Salim Ahmed Salim akiwa na viongozi waliodaiwa kuwa wa Hizbu miaka miaka ya nyuma.


 


Kutokana na picha hiyo Salim alikuja juu akisema kwamba picha hiyo na habari iliyoandikwa zililengwa kumharibia kisiasa ikizingatiwa kwamba zilikuwa zimebaki siku chache kabla ya uchaguzi kufanyika.


 


Wachunguzi wa masuala ya kisiasa wanaeleza kwamba, iwapo vyama hivyo vimeamua kupakana matope kwa njia hiyo basi suala la kufikia muafaka lisahaulike kwani uhasama kati ya vyama hivyo hautaiha bali daima utaendelea.


 


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents