MichezoUncategorized

Nani kuibuka mshindi michuano ya SportPesa Super Cup leo ?

Michuano ya SportPesa Super Cup inatarajiwa kuanza mapema hii leo kwa kuzikutanisha timu za AFC Leopard dhidi ya Singida United , huku Dar es salaam Young Africans ikicheza na mabingwa wa SportPesa Premier League klabu ya Tusker ya nchini Kenya.

Katika michuano hii mikubwa Afrika Mashariki inazikutanisha timu pendwa kutoka nchi mbili, Tanzania na Kenya, mashindano haya hayatofautiani sana na yale ya Emirates Cup ambapo klabu kama Real Madrid, Arsenal, AC Milan, S.L Benfica, Paris Saint-Germain, Olympiacos FC hushiriki licha ya kukabiliwa na michuano migumu katika ligi zao.

Wachezaji wa klabu ya Singida United wakiwa na mwalimu wao Hans Van der Pluijm

Historia fupi ya Singida United itakayo cheza na AFC Leopard ya Kenya 

Michuano hii inaleta mwamko mpya katika mchezo wa soka na kwa kiasi gani inaoneka kuzikutanisha pamoja baadhi ya timu za Kenya na Tanzania ambazo zinanguvu katika ligi zao na hivyo kutarajia kuona mashindano yenye msisimko na ushindani mkubwa ni wakati sasa kwa wachezaji kuonyesha uwezo wao ili kuyafanya kuwa bora zaidi.

Wachezaji wa klabu ya AFC Leopard ya Kenya wakiwa katika maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Singida United katika michuano ya SportPesa Super Cup

Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa wameingiza fedha nyingi katika mashindano haya na hivyo wangependa kushuhudia ushindani mkubwa katika michuano hii na kupata mafanikio wanayo yatarajia kwa ajili ya maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu nchini.

BY HAMZA  FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents