Michezo
Nani kuibuka mwanasoka bora? Ni Ronaldo, Messi au Neuer?
Fifa imetoa orodha ya mwisho ya wachezaji watatu wanaowania tuzo ya mwanasoka bora duniani maarufu kwa jina la FIFA Ballon d’Or 2014.
Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Manuel Neuer ndio wachezaji walioteuliwa kuwania tuzo ya FIFA Ballon d’Or 2014. Watatu hao ndiyo wameingia fainali na mshindi atapatikana Januari 12, 2015.
Wachezaji hao ni
Cristiano Ronaldo (Ureno/ Real Madrid),
Lionel Messi (Argentina/Barcelona) na
Manuel Neuer (Ujerumani/Bayern Munich)