Habari

Nani kuibuka Unique model leo Maisha Club?

Ile siku iliyosubiriwa na watanzania wengi kutaka kujua nani ataibuka mshindi wa shindano la kumsaka mwanamitindo wa mwaka mwenye sifa za pekee nchini Tanzania imewadia.

Homa ya shindano imezidi kupanda ikiwa usiku wa leo atajulikana nani atavishwa taji la unque model of the year 2012 taji lenye heshima katika tasnia ya mitindo nchini Tanzania.

Jumla ya washiriki kumi na mbili wanapanda kujwaani kuwania taji hilo ikiwa fainali zake zitafanyika katika ukumbi wa maraha New Maisha club uliopo Oysterbay jijini Dar.

Mratibu wa shindano hilo Methusela Magese amewaomba watanzania wajitokeze kwa wingi siku ya kesho kwani kuna mambo mazuri ya kufurahisha ikiwemo burudani ya muziki wa bendi toka kwa mashujaa,ngoma za asili na bongo flava kwa kiingilio cha Tshs 15,000/=

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents