Michezo

Nani kusajiliwa kwa dau la paundi 100m ?

Klabu ya Manchester United iliweka rekodi ya usajili wa paundi milioni 89 kumrudisha, Paul Pogba akitokea  Juventus mwaka uliopita je nani atakaye vunja historia hiyo.

Muda pekee ndiyo utakao zungumza ni nani atakaye weka historia ya usajili kwa msimu huu.

Real Madrid ilikuwa klabu ya kwanza kutoa dau la paundi ya zaidi ya milioni 50 wakati ilipomsajili mchezaji wa kimataifa wa brazili Kaka akisajiliwa kwa paundi milioni 56 akitokea AC Milan mwaka  2009, na Los Blancos hao kuvunja rekodi ya dunia mwaka 2009 kwa kumsajili Cristiano Ronaldo kwa dau la paundi milioni 80, na kisha kufanya hivyo mwaka 2013 kwa kumsajili aliyekuwa mchezaji wa Spurs, Gareth Bale kwa paundi milioni 86.

 

Lakini nani atakuwa wa kwanza kusajiliwa kwa dau la paundi milioni 100 ngoja tuone katika dirisha hili la usajili.

Kylian Mbappe

 

Rekodi inaweza kuvunjwa na kijana mwenye umri wa miaka 18  kutoka klabu ya  Monaco, Kylian Mbappe tetesi zikisikika kuwa bila ya dau la paundi milioni 100 hangoki

Inaripotiwa kuwa klabu za Hispania na Uingereza zimeenza kumnyemelea mchezaji huyo wa mabingwa wa ligi ya Ufaransa kwa dau la Paundi milioni 113.

Gareth Bale

Manchester United imeripotiwa kumtolea macho mchezaji huyo wa  Real Madrid  aliyeiwezesha kutwaa kombe la klabu bingwa barani Ulaya. Bale ana mkataba wa muda mrefu ndani ya klabu hiyo utakao kwisha mwaka 2022 na mwenye furaha kuwepo Santiago Bernabeu.

Eden Hazard

Raia huyo wa Ubelgiji mpaka sasa anawasikiliza Madrid kama watakuja kufanya naye mazungumzo au ataendelea kubaki Chelsea.

Romelu Lukaku

Mshambuliaji huyo ameuambia mtandao wa Sky Sport News HQ kuwa anafahamu anapoelekea katika msimu ujao wa ligi. “Wakala wangu anafahamu kinachokuja kutokea,” amesema.

Wakala wa mchezaji, Lukaku mwenye miaka 24 anaamini msambuliaji huyo anastahili dau la paundi milioni 100, kwa sasa amebakiza miaka miwili ndani ya Goodison Park.

Pierre-Emerick Aubameyang

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Gabon amesikika akihitaji kuondoka ndani ya Borussia Dortmund katika majira haya ya joto. “Kama nahitaji kufika mbali, nahitaji kuondoka kipindi hiki cha majira ya joto,” ameiambia Radio ya Ufaransa ya RMC.

Paulo Dybala

Mshambuliaji huyu wa Juventus ambaye alisaini mkataba wa miaka mitano lakini mwezi April, ametangaza kuondoka katika ligi ya Serie A na kutimkia Real Madrid ambayo imeonyesha nia ya kumtaka mchezaji huyo.

Dele Alli au Harry Kane

Harry Kane

Wachezaji hawa wa Tottenham Hotspurs mmoja wao anaweza kuachana na timu hiyo. Meneja Maurico Pochettino anapambana katika kuhakikisha wachezaji wake nyota wanaendelea kusalia kwenye timu hiyo.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents