Burudani

Nani zaidi kati ya Msondo na Sikinde, Jibu kupatikana Mei 20

Baada ya kutafutana kwa muda wa miaka miwili, hatimaye bendi hasimu za Msondo Ngoma na DDC Mlimani Park ‘Sikinde Ngoma ya Ukaye’ wanatarajia kuamua tena swali la nani zaidi, kati yao.

Mratibu wa pambano la Msondo na Sikinde, Abdulfareed Hussein akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam amesema, kwamba pambano linatarajia kufanyika tarehe Mei 20 mwaka huu, katika ukumbi wa Traventine Magomeni, Dar es Salaam. Bendi hizo zinatarajiwa kushindana kwa umahiri wa kuporomosha burudani ya muziki mzuri.

Akizungumza na waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam, mratibu wa mpambano huo, Abdulfareed Hussein alisema mpambano huo wa nani zaidi utaamuliwa na mashabiki wa dansi. Alisema kiingilio cha pambano hilo itakuwa ni Sh. 10,000 ili kuwapa nafasi wadau wa dansi kushuhudia na kutoa maamuzi ya nani zaidi kati ya bendi hizo mbili.

“Hili pambano ndio litakata mzizi wa fitna, ambapo mashabiki ndio wataamua nani zaidi kati ya Msondo au Sikinde,” alisema.

Wakati huo huo: Mmoja kati ya wawakilishi wa Sikinde, Abdallah Hemba alisema wamejiandaa vizuri kutoa burudani na kuhakikisha kwamba wako vizuri kuwashinda Msondo.“Hawa jamaa wametukimbia sana, hivyo kila tunapotaka kukutana nao wanakuwa na safari naona Mei 20 ndio mwisho wao,” alisema.


Baadhi ya wanamuziki wa bendi hizo wakitambulishwa.

Nao Meneja wa Msondo, Said Kibiriti,alisema wamejiandaa vyema katika pambano hilo na wataimba nyimbo mchanganyiko
“Tutaimba nyimbo mchanganyiko, na pia tutaimba nyimbo zetu mpya, tunaamini mpambano huo ndio utaweza kuamua nani kati yao ni zaidi,” alisema Kibiriti.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents