Burudani

Naomi aitwa Kortini

Mwanamitindo mwenye jina kubwa duniani na mwenye sifa ya kutokuchuja Naomi Campbell,amejikuta kwenye janga pale ambapo aliitwa korti la ‘The Hague’ nchini Netherlands bada ya kusadikiwa kupokea Almasi kutoka kwa kiongozi wa zamani wa Liberia Charles Taylor.

Charles Taylor hivi sasa anakabiliwa na kesi ya kupokea almasi za waasi wa nchi ya Sierra Leone na kubadilishana nao silaha zilizotumika katika mauaji na ubakaji wa wanawake na watoto katika nchi ya Sierra Leone. Rais huyo wa zamani amekanusha kabisa madai haya na kuapa kutowahi kupokea almasi za aina yoyote kutoka kwa waasi.

Naomi Campbell kuahidiwa almasi na Rais huyo walipokuwa katika hafla y chakula cha jioni iliyondaliwa na Rais Nelson Mandela mwaka 1997. Baadaye alisema kwamba wanaume wawili waligonga mlango wa chumba chake usiku n kumpa kitita chenye vijiwe vinne vichafu na kuambiwa kwamba ni Almasi kutoka kwa Charles Taylor.

Ms. Campbell alihakikishia mahakimu wa korti hiyo kwamba kama asingekubali kupokea mawe hayo kama angelijua ni ya waasi, na vilevile kuwa yeye ni Mwanamke mweusi wa asili ya Kiafrika hivyo asingeweza kukubali kusupport mauaji ya aina yoyote ya waafrika wenzake.

Naomi aliendelea kusema kwamba aligawa mawe hayo katika Nelson Mandela Foundation ili yaweze kusaidia kupata pesa na kuendeleza shughuli za taasisi hiyo.

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents