Habari

Nape aungana na Mhe. Kikwete, ‘wapinzani sio maadui’

Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye ametoa kauli ambayo inashabiana na aliyotoa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Kikwete kuwa wanasiasa wa upinzania sio maadui.

Katika kurasa zake za mitandao ya kijamii (twitter & instagram), Nape ameweka picha akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe na kuandika; “wapinzani sio maadui, tushindane kwa hoja’.

Kauli hiyo ya Nape inakuja siku chache baada ya Mhe. Jakaya Kikwete kushauri utawala barani Afrika kuheshimu sheria, huku akitaka wanasiasa wa upinzani wasichukuliwe na serikali kuwa ni maadui bali katika kuendeleza misingi ya demokrasia.

Pia aliongeza wabunge wa vyama tawala barani Afrika kuzikosoa serikali zao pindi wanapoona zinakwenda kinyume na ilani za uchaguzi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents