Habari

Nape Nnauye, Mo, Zitto na wengine waguswa na kifo cha mfanyabiashara Ali Mufuruki

Kifo cha Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania na Mfanyabiashara, Ali Mufuruki aliyefariki Dunia akiwa Afrika Kusini kimewashitua watu wengi akiwemo bunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye, mfanyabiashara Mohammed Dewji, Zitto kabwe na watu wengine.

Aliyekuwa Mfanyabiashara maarufu Tanzania, Ali Mufuruki.

 

Mbunge wa Kigoma Mjini, na kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, ameonesha kupokea kwa masikitiko makubwa kufuatia kifo cha Mfanyabiashara maarufu hapa nchini, Ali Mufuruki, aliyefariki Dunia akiwa nchini Afrika ya Kusini.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Kijamii wa Twitter, leo Desemba 8, 2019, Zitto, ameandika maneno yaliyoonesha ni kwa namna gani, alikuwa akimfahamu mfanyabiashara huyo.

“Sina maneno ya kusema zaidi ya kuwa sote ni wake Mwenyezi Mungu na kwake sote tutarejea, sio tu alikuwa rafiki bali alikuwa mshauri wangu, tulipishana mawazo fulani lakini alikuwa na heshima kubwa, tangulia ndugu yangu RIPMufuruki” ameandika Mbunge Zitto Kabwe.

Mwanasiasa mwingine aliyeonesha kuguswa na msiba wa Ali Mufuruki ni mwanasiasa wa muda mrefu Khamis Kagasheki, ambaye ameandika hivi.

“Kwa mshtuko na masikitiko nimepata taarifa kwa kifo cha Ndg Ali Mufuruki, pigo kubwa kuondokewa na Ali, mkono wa pole nyingi kwa familia yake, MwenyeziMungu amhurumie na amsamehe. Ali you will be missed immensely”.

Ali Mfuruki aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Vodacom Tanzania, aliyehudumu kwa muda wa miaka miwili, ambapo baadaye alitangaza kujiuzulu nyadhifa zake zote kuanzia Agosti 1, 2019.

Mohamed Dewji (Mo)

Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un. Pumzika kwa amani Mzee Mufuruki! Tangulia nasi tunakuja. Hii safari yetu sote 🙏🏽

https://www.instagram.com/p/B5zZ_jClc7d/

Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye

Ni kazi ngumu sana kusimamia kile unachoamini hasa kama kitendo hicho kitakufanya msielewane na marafiki na watu wako wa karibu, LAKINI wewe Ally Mfuruki uliweza kuwa imara na mkweli kwa ulichoamini! Pumzika kwa amani!

Wengine walioguswa na kutuma salamu za pole kwa ndugu jamaa na marafiki wa mfanyabiashara huyo ni pamoja na Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents