Habari

Napiga marufuku magari ya chanjo kutumika kwa shughuli tofauti – Waziri Ummy

Serikali imezipiga marufuku halmashauri zote nchini, kutumia magari ya chanjo kwa matumizi mengine na kwamba kuanzia sasa yataandikwa kwa maandishi makubwa ili yaweze kutofautishwa na magari mengine.

Marufuku hayo yamepigwa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto, Mhe Ummy Mwalimu, Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mvomero, Sadiq Ahmed Murad lililohoji,

Gari la Afya ambalo linatumika kwaajili ya chanjo, leo hii linatumika kwaajili ya kukusanyia mapato, lakini idara ya ujenzi haina gari magari yote ni chakavu, Je, Muheshimiwa Waziri uko tayari watu wa Mvomero ili tuweze kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano?

“Natumia bunge hili kupiga marufuku magari ya chanjo kutumika kwa shughuli tofauti na chanjo na kuanzia sasa hivi magari ya chanjo tutayaandika kwa herufi kubwa ili lisitumike kwa matumizi mengine yoyote kwasababu chanjo ni muhimu kuliko matumizi mengine katika halmashauri . Muheshimiwa spika nikaona nitumie Bunge lako tukufu,” amesema waziri Ummy.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents