Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Nas na Nick Minaj wafanya kweli!

Kumeendelea kuwa na utata juu ya mahusiano yaliyopo kati ya rapper Nas na mwanadada Nick Minaj kufuatia mabusu waliokuwa wakipigana hadharani katika birthday ya Nas iliyofanyika usiku wa tarehe 13/8 mwaka huu.

Sherehe  hiyo iliyoudhuliwa na mastaa kama  Alicie Keys, Swiz Beat na wengineo, huku rapper huyo wa kike anayefanya vizuri kwa sasa na ngoma ya ‘You Already Know’ aliyoshirikishwa na Fergie,  akiwa karibu zaidi na Birthday boy na kufanya watu kupata mshangao baada ya picha zao na video  kuzagaa mtandaoni.

Mwezi Mei mwaka huu wawili hao waliwahi kuwa katika mgahawa wa Sweet chick mjini NYC, na mikao yao ikaanza kuleta utata, mrembo huyo kutoka Young Money hajawahi kuficha upendo wake kwa Nas, na hata kufikia hatua ya kumshirikisha kwenye video yake ya ‘Right By My Side’ wimbo ambao unawaonyesha wawili hao wakiwa na hisia kali sana.

Kabla ya kuonyesha ukaribu aliyonao kwa Nas, mrembo huyo aliwahi kuwa na mahusiano  ya kimapenzi na rappper Meek Mill ambao wameachana toka mwezi wa kwanza mwaka huu.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW