Burudani

Nasikitika kuona watu wanatafuta habari za uongo – Madam Flora

Muimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania, aliyekuwa mke wa Emmanuel Mbasha (Madam Flora) anasikitika kuona watu mpaka sasa wanatafuta habari za uongo baada kuenea habari kuwa yeye amezungumza na chombo cha habari ambacho hata jina lake halitambui kuwa kama mwanaume hakuridhishi hakufai amesema habari hizo si za kweli.

Madam Flora ameongea na  Bongo5 Jumatano hii,  amefunguka kuwa ni vyema watu hao wakatafuta maisha kuhakikisha kwamba wanaishi maisha mazuri ili kuhakikisha watoto wao wanasoma vizuri.

“Nilizipokea hizo habari nilijisikia vibaya unajua mtu akalala akaamka tu na Madam Frola kwamba Frola amesema moja mbili tatu kwamba alikuwa anahojiwa na kituo fulani cha redio na redio yenyewe siijui iko wapi, sijawahi hata kuisikia ndo kwa mara ya kwanza nikajua hapa Tanzania kuna redio kama hiyo inaitwa sijui ni swahili, sasa kwa kweli inasikitisha lakini unakuta labda mtu ana mambo yake kichwani labda anatafuta followers kwenye page yake,” amesema Madam Flora.

Ameongeza “Labda tu ameona aandike kwa maslahi yake binafsi na anategemea akiandika hivyo ndio anapata kula ili asikose chakula cha watoto inabidi tu aandike ujinga na uongo kupitia kitu fulani sasa inakuwa sio nzuri kwa kweli nilisikitika sana kuona watu kwa kipindi hiki wanatafuta habari za uongo uongo kuziposti kwenye page zao baada ya kutafuta maisha kuhakikisha kwamba wanaishi maisha maziri ili kluhakikisha watoto wao wanasoma vizuri yani mtu amekaa kutafuta umbea ambao haumsaidii it’s to bad kwakweli.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents