Habari

Nassari atema cheche kwa mara ya kwanza tangu avuliwe ubunge, amtaka Spika arejee upya maamuzi yake (video)

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amesongea leo kwa mara ya kwanza tangu Spika Ndugai atangaze kumfuta ubunge kwa kushindwa kuhudhuria vikao vitatu vya Bunge mfululizo.

Nassari akiongea leo Jumapili Machi 17, 2019 mbele ya waandishi wa habari, amekiri kuwa ni kweli Mwezi Novemba 2018 na Januari 2019 hakuhudhuria vikao vya Bunge kwa kuwa alikuwa na matatizo ya kifamilia.

Ameeleza kuwa mke wake alikuwa na matatizo ya kiafya, ambapo alihitaji uangalizi wa karibu wa kifamilia yake ambapo mkewe alienda kutibiwa nchini Marekani .

Nassari amesema mnamo Januari 27, 2019, mke wake alijifungua mtoto nchini Marekani na kesho yake Januari 28 vikao vya Bunge vilikuwa vinaanza na kumuacha na machaguo mawili, kuhudhuria Bunge au kumuuguza mkewe na yeye alichagua kumuuguza kwanza mkewe.

Hata hivyo, licha ya kuchagua kumuuguza mkewe, Nassari amedai kuwa aliandika barua kwenda kwa Spika kupitia anuani aliyopewa na Msaidizi wa Spika ili kumueleza matatizo anayopitia yeye na famialia yake.

Kwa upande mwingine, Nassari amesema kuwa ana haki ya kuulizwa au kuhojiwa na ofisi ya Bunge, kwa kutohudhuria bungeni na pia anamini Spika kama mzazi au mlezi wa Bunge ana uwezo wa kurejea maamuzi yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents