Burudani

Nataka kufanya kazi na ‘dogo’ kama Luffa – JCB

Msanii wa Hip Hop Bongo, JCB baada ya kurejea Bongo kutoka barani Ulaya ameeleza mipango yake kwa sasa.

JCB amesema anataka kurudi katika game ya Bongo Flava na maprodyuza wote aliokuwa akifanya nao kazi wanamsubiri waanze kazi ila anashawishika zaidi kufanya na Luffa.

“Sema nataka kufanya kazi na dogo kama Luffa, sijawahi kukutana nae wala simjui lakini nampa respect na ninataka kukutana nae kufanya kitu nae,” JCB ameimbia Clouds Fm na kuongeza.

“Nimenunua studio kule Ulaya nimekuja na studio yangu nataka niiweke pale Arusha, itakuwa ni home studio sio studio ya biashara nataka nifanya mazoezi nimrejeshe JCB, nirekodi ngoma kibao then nitarudi.,” amesisitiza.

JCB aliwahi kushinda tuzo ‘KTMA’ kupitia ngoma yake ya Ukisikia Paah Remix ambayo iliwakutanisha wasanii kama Chid Benz, Jay Moe na Fid Q.

By Peter Akaro

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents