Habari

Nataka kujua Prof. Lipumba amepatwa na nini – Gwajima

Kauli hiyo ya Askofu Gwajima imekuja baada ya kumaliza mazungumzo na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif ambaye alikuwa na ziara katika Kanisa la Askofu huyo. Baada ya mazungumzo hayo, waandishi wa habari walitaka kujua mazungumzo yao yalikuwa ni nini haswa.

“Mimi huyu ni rafiki yangu. Kwa hiyo nilitaka kujua Professa Lipumba anafanya nini kuvuruga CUF, hivyo nilitaka kujua Lipumba amepatwa na nini, mpaka amevuruga chama chao na kiukweli mimi nilikuwa siufahamu vizuri huu mgogoro ila sasa Seif ameniambia kwa hiyo na mimi nataka nitafakari alichoniambia rafiki yangu ni ‘digest’ baada ya hapo nitajua nitafanya nini” alisema Gwajima

Nae Maalim Seif Sharif Hamad alisema kuwa, amekaa na askofu Gwajima na kuzungumza naye kwa kina juu ya mgogoro huo.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents