Uncategorized

Nataka maaskari wetu wawe na nyumba nzuri na zisiwe zile nilipokwenda kuposea mlango gunia, natambua kazi nzuri mnazofanya – Rais Magufuli (+video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.John Pombe Magufuli hii leo amefungua mafunzo ya Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Polisi jijini Dares Salaam huku akiwapongeza kwa kazi nzuri wanazozifanya na kuwahasa kusimamianidhamu, maadili na kuzingatia majukumu yao katika uchaguzi wa Serikali zaMitaa unaotarajiwa kufanyika hapo mwakani 2019 na kuwaahidi kuimarisha makaziya maaskari.

‘’Niseme kwa dhati hapa ni marayangu ya kwanza kuweza kuja, lakini nilikuwa napafahu, nimarayangu ya kwanza kuja nikiwa Rais, ninapafahamu kwa sababu gani?, jeshi la Polisi nyinyi ni wakwe zangu, nimeoa kwenye kambi kwahiyo amri amri hizo nimezizoe,’’ amesema Rais Magufuli

Dk. Magufuli ameongeza ‘’Nataka niwaambie, mimi kiongozi wenu ninatambua kazi nzuri mnazofanya, msivunjike moyo endeleeni kuchapa kazi, Mh IGP ninakupongeza sana na makamanda wote kweli mnafanya kazi nzuri sana’’

‘’Ninapitia orodha yangu ya mapendekezo mbalimbali, ambao baadhi pia ya maaskari nitawapandisha haraka, kwamfano yule wa Mwanza na ‘group’ lake la watu 27 aliyowalaza chali pale watu, lazima nimpongeze kakiwepo kanyota kamebaki ninakapandisha hapo hapo.’’

‘’Ninachotaka kuwaambia Jeshi la Polisi mnafanya kazi nzuri sana, ninakumbuka Mwanza wakati fulani Kamanda aliyekuwepo kule, watu wamechinjwa hadharani Msikitini, watu wakauawa alienda kushambulia pale na akawapata wauaji.’’

Kwa upande mwingine Rais amesema ‘’Ninawapenda sana tembeeni kifua mbele, Mh IGP na Naibu Waziri wameeleza hapa baadhi ya hatua tunazozichukua za kuhakikisha kwamba jeshi letu tunaliimarisha kwakuleta vifaa makazi ya nyumba.’’

‘’Ninataka maaskari wetu wote wakiwemo na wajeshi la Polisi wawe na nyumba nzuri, zisiwe zile nyumba nilipokwenda kuposea, ambapo mlango ni gunia, ni lazima tubadilishe hii hali na mimi nataka niwahakikishie kwamba nipo pamoja na ninyi’’

‘’Kabla sijahitimisha hutuba yangu, napenda nitumie fursa hii kusema kwa dhati kuwa Serikali inatambua kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Jeshi la Polisi nchini na nidhamira yetu kuona Jeshi hili linaendelea kufanya kazi zake kwa weledi na kisasa zaidi.’’

‘’Mwisho kabisa napenda kuwakumbusha Jeshi la Polisi kuwa hivi sasa, tumebakiza siku chache kuingia mwaka 2019 ambao ni mwaka wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa.’’

‘’Kama mnavyofahamu ingawa chaguzi ni mchakato muhimu katika kukuza Demokrasia ya nchi yetu, nyakati nyingine zinakuwa chanzo cha vurugu na kuvunjika kwa amani katika Taifa, mifano inayotokea kwa baadhi ya nchi zingine.’’

‘’Kwahiyo niwaombe Jeshi la Polisi kasimamieni nidhamu, kasimamieni maadili, kazingatieni majukumuyenu katika kuhakikisha tunamaliza chaguzi hizi tukiwa salama na tukiwa wamoja.’’

Rais Magufuli amesema siku zote amekuwa akizungumza kuwa  Jeshi la Polisi linaumuhimu mkubwa  katika usalama wa Watanzania na kuongeza kuwa vyombo vya ulinzi vinaumuhimu mkubwa katika kulinda hata rasilimali zetu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents