Michezo

Natamani ‘Boyfriend’ ila wanaume wananiogopa – Asema mwanamke mnyanyua vyuma

Mwanamke mnyanyua vyuma maarufu nchini Urusi,  Natalia Kuznetsova amesema kuwa anatamani kuwa na mchumba atakayemuoa baadae lakini wanaume wengi wamekuwa wanamuogopa kumtongoza.

Natalia Kuznetsova

Natalia Kuznetsova (26) ambaye alianza mazoezi akiwa na miaka 14 amesema alishawahi kuolewa na mwanaume ajulikanaye kwa jina la Vladislav Kuznetsov kipindi akiwa na miaka 20 lakini hakudumu nae kwa muda mrefu.

Akieleza sababu za kutodumu nae amesema kuwa rafiki yake huyo alikuwa hapendi watembee pamoja mtaani akiogopa kuchekwa na hiyo ni baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa kuongeza kifua.

Kila mwanamke duniani ni mzuri siamini kuwa nikiwa mwanamichezo basi nitakosa mwanamme wa kunioa.“amesema Natalia kwenye mahojiano yake na kituo cha runinga cha Raptly TV huku akielezea safari ya mahusiano yake.

Nilishawahi kuolewa kipindi nikiwa na miaka 20 nilimpenda sana mume wangu lakini haikuwa bahati yangu kwani alikuwa ananionea aibu hakutaka niongozane nae, pengine baada ya kufanya upasuaji wa kuongeza kifua changu. Mimi ni mwanamke kama wengine natamani sana kuwa na mchumba kwa sasa ikibidi tuoane, bado naamini wapo wanaume wengi wananipenda ila labda wanaogopa muonekano wangu nilivyo.“amesema Natalia.

Natalia ambaye mwaka jana alitangaza kustaafu mchezo huo na kubaki kama kocha, wiki hii ametangaza kurudi tena uwanjani kama mchezaji.

Hata hivyo mrembo huyo mwaka 2015 alikiri wazi kuwa anajihusisha na mapenzi ya jinsia moja baada ya kuishi muda mrefu bila mwanaume.

Mrembo huyo mwenye umbo la kibabe  ameshinda tuzo kibao nchini Urusi na nyingine za kimataifa za kunyanyua vyuma vizito.Tazama mahojiano yake na Raptly TV.

Natalia ana kilo 90 na anapatikana kwenye mtandao wa Instagram mfuate kwa jina hilo hilo na hapa chini ni baadhi ya picha zake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents