Habari

Natambua nchi ina uhaba wa wataalam wa afya – Mhe. Mkapa

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa amesema anatambua kuwa nchi ina uhaba wa Wataalamu wa afya huku akiwataka kwa wale wachache wenye dhamana ya afya kufanya kazi kwa tija na ufanisi.

Mhe. Mkapa ameyasema hayo Jumatatu hii, wilayani Chato wakati akimkabidhi Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu Hati ya umiliki wa Nyumba 50 za Watumishi wa Afya katika Mikoa ya Geita, Kagera na Simiyu, Zilizojengwa na Taasisi yake ya Mkapa Foundation.

“Natambua kwamba nchi yetu bado ina uhaba wa Wataalamu wa afya, lakini kwa wale wachache wenye dhamana ya huduma za Afya hamna budi kujituma na kuwa wabunifu zaidi kufanya kazi kwa tija na ufanisi kwa uchache wenu kuzingatia na kufuata maadili ya taaluma zenu,” alisema Mhe. Mkapa.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents