BurudaniHabari

Nature kuwapa vyeo Dollo, Karama, D. Chief na BFK & Q

Sir Nature‘Sir Nature’ amesema kuwa, akiwa kiongozi wa kundi la Wanaume Halisi amepanga kuwainua wasanii wachanga na kuwapa hadhi na majina kama ilivyo kwake yeye.

Msanii nyota Juma Kassim ‘Sir Nature’ amesema kuwa, akiwa kiongozi wa kundi la Wanaume Halisi amepanga kuwainua wasanii wachanga na kuwapa hadhi na majina kama ilivyo kwake yeye.

 

Akizungumza na Tanzania Daima hivi karibuni, Sir Nature alisema kundi la Wanaume Halisi ambalo linaundwa na wasanii waliojiengua kutoka katika kundi la Wanaume Family la Temeke ‘TMK’, lakini hawakupata majina hivyo wamepanga kuwapa nafasi ya kutamba na kufahamika kwenye fani.

 

Nature aliwataja wasanii ambao amepanga kuwapa nafasi kubwa ambayo walipokuwa kwenye kundi la TMK waliikosa kuwa ni Luteni Karama, Dollo, BFK & Q na D. Chief.

 

“Hii ni njia mojawapo ya kuwatoa na nitawapa nafasi kubwa ya kuonyesha umahiri wao wa kutunga na kuimba, huu si wakati wa kubaniana kwani sote tunatafuta maisha mwanangu,” alisema.

 

Pia kundi la Wanaume Halisi litazindua nembo yao hivi karibuni ambayo itakuwa ikiwatambulisha popote watakapokuwa.

 

Kundi hilo limepanga kuzindua albamu yake mwishoni mwa mwezi huu, ambapo pia watakuwa wakicheza katika mtindo wa ‘Kung Fu’, kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Upanga Dar es Salaam.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents