Habari

Nauli ya ndege kama ya basi!! FastJet kuanza safari zake kwa kishindo

Kampuni ya ndege ya FastJet imeanza rasmi kuuza tiketi za ndege kwa safari za ndani ya nchi ambapo safari zitaanza November, 29.Kilimanjaro na Mwanza ni mikoa ya kwanza kwa safari hizo.

Habari njema ni kuwa nauli ya ndege kwaajili ya safari hizo hazina tofauti na zile za mabasi yaendayo mikoano ambapo tiketi moja inauzwa kwa shilingi 32,000($20) bila kodi.

FastJet imefungua ofisi zake jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza barani Afrika ambapo kituo cha pili kufunguliwa siku za usoni kitakuwa jijini Nairobi, Kenya ikifuatiwa na Accra, Ghana na Luanda, Angola.

Mwenyekiti mtendaji wa FastJet Ed Winter alisema hiyo ni hatua ya kihistoria kwa usafiri wa ndege nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.

“Air travel is no longer an exclusive option for a small minority in Tanzania. FastJet will make flying an affordable option for more Tanzanians than ever before, bringing new opportunities for trade, leisure trips, and family visits,” alisema.

FastJet ilichukua nafasi ya kampuni ya Fly540 yenye makazi yake jijini Nairobi mwezi June mwaka huu baada ya kampuni mama ya Lonrho Aviation kuamua hivyo.

Fly540 tayari imeacha kutoa huduma jijini Dar es Salaam ili kupisha uzinduzi wa FastJet.

FastJet itaanza kutoa huduma kwa ndege zake tatu aina ya Airbus A319s, ambapo baada ya miezi 12 kutakuwa na jumla ya ndege 12. Hadi mwaka 2016 kampuni hiyo inatarajia kuwa na ndege 40..

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents