Habari

Nauli zawachanganya wamiliki wa mabasi

MABASI yaendayo mikoani kutoka Dar es Salaam bado hayajatangaza nauli mpya, licha ya Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) kuridhia kupanda kwa nauli za mabasi hayo kwa kiwango kinachoanzia Sh 25 kwa kilomita moja kwa mabasi ya kawaida, imefahamika.

Waandishi Wa Habari Leo


MABASI yaendayo mikoani kutoka Dar es Salaam bado hayajatangaza nauli mpya, licha ya Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) kuridhia kupanda kwa nauli za mabasi hayo kwa kiwango kinachoanzia Sh 25 kwa kilomita moja kwa mabasi ya kawaida, imefahamika.


Sanjari na hilo, wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wamelalamikia up andaji wa nauli mpya za
daladala, ambazo baadhi zimekuwa zikiwalipisha nauli za juu viwango vilivyoridhiwa na
Wakizungumza na gazeti hili jana kwa nyakati tofauti, walisema kupanda kwa nauli ni kero kwa watu wenye kipato kidogo.


Mkazi wa Mbagala Kizuiani, anayefanya shughuli zake Mwenge, Asha Abdallah, alisema ongezeko hilo la nauli jana lilisababisha vurugu kwenye Kituo cha Mbagala kutoka
kwa abiria kwani kabla nauli hazijapanda, walikuwa wakitozwa Sh 300, lakini kwa sasa ni Sh 350 na inahofiwa kufikia Sh 400, majira ya kuanzia saa moja jioni.


Mkazi mwingine wa Mbagala Charambe, aliyejitambulisha kwa jina moja la Abdallah, alisema makondakta na madereva wanapandisha nauli kwa sababu zao binafsi kwani vituo
vya katikati, bado wanatoza nauli kati ya Sh 350 bila kujali umbali.


Alisema nauli hiyo si sawa kwani kwa mujibu wa Sumatra, wanatakiwa wachukue Sh 200 kwa sababu abiria wanashukia njiani hawafiki mwisho wa safari. Baadhi ya wanafunzi walisema ingawa serikali imesema walipe Sh 50, lakini wanaendelea kunyanyaswa na makondakta kwa kusukumwa wakati wakigombea kupanda daladala kwenda shule au kurudi nyumbani na
wakati mwingine kuachwa vituoni.


Hata hivyo, mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Sinza, Elizabeth Mbwana, alisema akondakta wanaona Sh 50 anayotoa mwanafunzi, haina faida kwao hivyo wanawaacha vituoni na kuchukua watu wazima bila ya kujali kama wanafunzi wanachelewa shule.


“Serikali iweze kutuletea magari ya wanafunzi ili kuepukana na matatizo haya ya usafiri nchini kwani wanafunzi tunanyanyasika,” alisema Elizabeth. Viwango na nauli ya daladala ilivyoridhiwa na Sumatra ni ongezeko la Sh 50 kwa umbali mfupi ambapo nauli mpya ni kati ya Sh 250 badala ya Sh 200 wakati Sh 300 badala ya Sh 250 ni kwa umbali wa kati, na za
umbali mrefu ni Sh 350 badala ya 300 na pembezoni mwa Jiji ni kati ya Sh 400 na Sh 500.


Sumatra ilitangaza viwango vya nauli baada ya kupokea mapendekezo ya nauli mpya za mabasi kutoka kwa Chama cha Wamiliki wa Daladala (DARCOBOA) na Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) na kuyafanyia kazi na kuridhia kupanda kwa nauli.



Mamlaka hiyo ilizitaja sababu za kupanda kwa nauli kuwa ni kupanda kwa bei za mafuta, mfumuko wa bei pamoja na gharama za uendeshaji. Mkurugenzi wa mabasi ya Dossa Trans yanayofanya safari zake kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya, Morogoro, Dodoma, Mwanza na Kahama, alisema Sumatra wanapaswa kuainisha kiwango cha nauli kama walivyofanya
kwenye mabasi ya daladala.


Alisema wanashindwa kuamua kiwango gani waongeze kwani inaweza kuwa ni usumbufu kwa abiria, wakati mwakilishi wa Kampuni ya mabasi ya Ngalaiya Express, Ngonyani Kidukuli, alifafanua kuwa wanasubiri mamlaka hiyo ijadiliane na wenye mabasi na kutangaza kiwango
kinachotakiwa na kuwatangazia abiria.


Watumishi wa mabasi ya mikoaniwalisema hawajapata maelekezo kutoka kwa waajiri wao, hivyo viwango vya nauli vimebaki vya awali hadi wamiliki watakapotoa tamko rasmi.
Baadhi ya wasafiri waliokuwa safarini jana, walieleza kuwa hawakulipishwa nauli mpya, hali inayoonyesha kuwa viwango hivyo vilikuwa havijaanza kutumika.


Mwalimu Briton Mwakalebela wa Shule ya Msingi Manzese, ambaye alikuwa akitoka Mbeya, alisema alijiandaa kwa mabadiliko ya nauli, ingawa hakufahamu kiasi gani cha nauli ambayo anastahili kulipa.


Mwakalebela alisema alipofika kituo cha mabasi ya Hood, alikuta nauli haijapanda kwani nauli ya Mbeya kwenda Dar es Salaam ilikuwa ile ile ya Sh 15,000.


Naye Mwanamkasi Shabani aliyekuwa akitokea Korogwe mkoani Tanga kwenda Dar es Salaam, alisema nauli haijapanda kwani wanalipa Sh 8,000, aliyolipa jana.


Aidha, James Mnanzila aliyekuwa akienda Kahama, alisema nauli ya kwenda huko ni Sh 32,000, kiwango ambacho ni cha zamani. Alisema alikuwa tayari kulipa nauli mpya kama vilivyokuwa vimetangazwa.


Source: Habari Leo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents