BurudaniVideos

Navio: Tunafanya collabo na wasanii wa nje na kuwapa nguvu zaidi (Video)

Rapper wa Uganda, Navio ametaka kuwepo na ushirikiano zaidi kwa wasanii wa Afrika Mashariki ili kuufanya ukanda huu uwe na nguvu zaidi.

navio-21

Akiongea na mimi jijini Lagos alikokuwa ameenda kuhudhuria tuzo za Afrima, Navio amesema kwa kuendelea kufanya collabo na wasanii wa nje, wanajikuta wao wanakuwa wakubwa zaidi kuliko wa Afrika Mashariki.

“Ni kama tunafanya collabo sana na wasanii wa nje na kuwafanya wawe wakubwa. Wasanii wote wa Afrika Mashariki wanataka kufanya kazi na wasanii wa Nigeria na mwisho tunaishia kuwafanya wanakuwa wakubwa zaidi,” amesema Navio.

“Nataka kumuona Joh Makini akifanya kazi na The Mith, nataka kumuona Khaligraph akifanya kazi na rapper wa Rwanda. Tukiwa na kitu kama hicho, na tukawa na mashabiki wetu wa utamaduni wa hip hop tutafanikiwa.”

Mtazame zaidi kwenye interview hiyo juu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents