Burudani ya Michezo Live

Navy Kenzo: ‘Chelewa imetupa nguvu’ waeleza maana ya jina lao na mipango ya 2014 (Video)

Kundi la Navy Kenzo limesema wimbo wake mpya, Chelewa umelifungulia njia na kuwapa mafanikio kuliko nyimbo zake zingine. Wakiongea na Bongo5, Nahreel na Aika wanaounda kunda hilo la wasanii watatu wamesema mapokeo ya wimbo huo yamewapa moyo.

“Chelewa ni wimbo ambao umetupa energy sana kutengeneza vitu vingine,” alisema Nahreel. Naye Aika alisema kinachofuata ni video ya Chelewa. Akiongelea maudhui ya wimbo huo, Aika amesema Chelewa ni wimbo ambao mwanaume anamlalamikia mpenzi wake anayemchelewesha kumuoa.

“Mwanamke anamuimbia ‘sisi kwenye familia yetu kuna mila na desturi na mambo mengine ambayo unabidi ufuatilie kwanza ndio uweze kunioa,” alifafanua Aika.

Akielezea maana ya jina lao Navy Kenzo, Nahreel alisema:

Navy Kenzo ni maneno mawili, Navy na Kenzo. Navy ni neno la Kiingereza la kawaida ambalo linamaanisha jeshi au army, kama kikundi flani cha upiganaji. Halafu Kenzo ni neno la Kijapan ambalo linamaanisha watu watatu wenye busara, hivyo Navy Kenzo ni ‘Jeshi la watu watatu’.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW