BurudaniVideos

Navy Kenzo wakusanya kijiji Tel Aviv, Israel, washangazwa na jinsi wanavyokubalika

Kundi la muziki la Navy Kenzo jana wameanza tour yao iliyopewa jina la Aim World Tour katika nchi tofauti duniani. Hiyo jana walifanikiwa kufanya show yao ya kwanza pale mjini Tel Aviv nchini Israel.

Akizungumza na kipindi cha Extra Fleva KInachoendeshwa na Ergon Elly, Aika kutokea nchini Israel amesema kuwa wameshangazwa na mapokezi makubwa ya kazi zao.

Amesema kuwa fursa hiyo watatumia kufanya video za kazi yao Feel Good remix waliyomshirikisha Dj Moshe na siku ya jana member hao wa Navy Kenzo walifanikiwa kumtembelea Dj moshe katika studio zake na tayari wameanza kufanya kazi nyingine na Moshe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents