Burudani

Navy Kenzo waumia kuona nyimbo kutoka kwenye albamu ya ‘AIM’ zinasambazwa mitandaoni

Msanii wa Kundi la Navy Kenzo, Aika ameonyeshwa kusikitishwa na kuvunjwa moyo na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakizivujisha nyimbo kutoka kwenye albamu yao mpya ‘AIM’ na kuzisambaza mitandaoni.

Muimbaji huyo alidai kitendo cha baadhi ya watu hususani bloggers kuchukua nyimbo hizo kwenye albumu na kuziweka mitandaoni kinakuwa kinawavunja moyo kwani kinasababisha biashara yao kupunguza kasi na kuharibu mauzo ya album hiyo mtaani.

“Inasikitisha sana pale msanii unapofanya kitu kikubwa halafu baadaye mtu anaitoa bure kazi yako, sisi kama Navy Kenzo tumefanya kazi kubwa sana mpaka kukamilisha hiyo kazi, tumethubutu, sasa unapoona blogs zinaweka zinatuharibia biashara hata watu wanaonunua albamu wakiona tena mtandaoni wanajisikiaje,” Aika alikiambia kipindi cha EA Radio.

Muimbaji huyo alisisitiza kuwa anatambua bloggers huenda wanajua wana wa’support’ kwa ku-upload nyimbo hizo kwenye mitandao ya jamii ili kusaidia albumu kuuzika lakini huenda wengine hawajui kile wanachofanya kinawaharibia wao soko la albumu yao mtaani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents