Aisee DSTV!

Navy Kenzo wazungumzia album mpya, ‘Niroge na wimbo mpya ‘Moyoni’

Kundi la Navy Kenzo linajiandaa kuachia wimbo wake mpya ‘Moyoni’ wiki hii huku pia likijiandaa kutoa album mpya, ‘Niroge’ mapema mwakani.

928070_755813884497437_1927403882_n

Procuder Nahreel amesema maandalizi ya album mpya yako mbioni kufikia tamati.

“Hii album itatoka January mwakani, maandalizi ni mazuri mpaka sasa hivi, nyimbo nane tayari, ambazo katika nyimbo nane hizo moja wapo tumemshirikisha Joh Makini,” Nahreel ameiambia Bongo5. “Kwahiyo album itakuwa na nyimbo tisa au kumi. Pia katika hii album utamsikia Christian Bella.”

Kuhusu wimbo wao mpya ‘Moyoni’, Nahreel amesema utakuja na video yake.

“Moyoni inazungumzia mtu umemweka moyoni mwako na unampenda na video itafuatia. Iko tofauti sana kwasababu tulishoot Arusha. Tulishoot maeneo ambayo wanaishi wamasai, kwahiyo itakuwa video nzuri. Audio itatoka kesho Mungu akipenda na video tumeona itoke ijumaa ili kupishanisha.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW