Burudani

Nay wa Mitego aeleza sababu za kutoa video ya ‘Sina Muda’ akiwa bado na deni la video ya ‘Mapenzi au Pesa’

Msanii wa muziki Nay Wa Mitego, Jumapili ya kesho (July 12) anatarajia kuachia video ya wimbo wake mpya ‘Sina Muda’, wimbo uliofata baada ya ‘Mapenzi au Pesa’ aliyomshirikisha Diamond.

nnnay

Nay ameleeza kwanini ameamua kutoa video ya wimbo mwingine kabla ya kutoa video ya ‘Mapenzi au Pesa’ iliyotangulia kutoka.

“Unajua Mapenzi au Pesa ilibidi iwe imeshaisha na iwe imeishatoka,” Nay Wa Mitego ameiambia Bongo5. “lakini kama unavyojua hapo katikati Diamond alikuwa anapilika nyingi halafu mimi mwenyewe pia nilikuwa sijatulia mambo yalikuwa mengi.”

Amesema kuwa wimbo wa ‘Sina Muda’ haukuwepo kwenye mipango ya kutoka lakini mapokezi yake ndio yamemshawishi kuifanyia video, na kuongeza kuwa video za Hip Hop ni rahisi zaidi kufanya.

“Uzuri wa hii imekuwa ni video moja nyepesi sana kama unavyojua video za hip hop zinakuwaga ni simple sio complicated sana. Haikuwepo kwenye ratiba nimeifanya tu fasta na nikaona ni wimbo tayari unatembea kwa nguvu yaani wenyewe unatembea bila hata kusukumwa, nikaona ngoja niupush kwa video lakini video ya Mapenzi au Pesa Jumatano tunashoot .”

Kuhusu kama haoni kuachia video mbili kunaweza kusababisha kuipunguzia nguvu ile atakayotangulia kuitoa hiki ndicho alisema Nay;

“Unajua hii ni miziki miwili tofauti, so sidhani kama inaweza zikaathiriana lakini mwisho wa siku nafikiri zitapeana kama wiki mbili tatu, mapenzi au pesa ikiisha nafikiri ndani ya wiki mbili baada ya kuachia hii, so hii Jumapili inatoka ile itakuwa inayofata.”

‘Sina muda’ ambayo inatoka kesho imeongozwa na Director aitwaye Joowzey, na ‘Mapenzi Au Pesa’ itaongozwa na Hanscana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents