Burudani

Nay wa Mitego afunguka baada ya kuhojiwa na polisi ‘nipo salama jamani’

Rapper Nay wa Mitego amefunguka na kuzungumzia issue ambayo imemfanya ahojiwe na jeshi la polisi na baadae kuachiwa kwa dhamana.
Nay wa Mitego

Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii, Nay amesema kitu ambacho kimemfanya ahojiwe na polisi hakihusiani na maswala ya muziki.

“Kweli bhana nimehojiwa na nipo nje kwa dhamana,” alisema Nay wa Mitego. “Siyo issue za muziki ni maswala yangu binafsi, na nisingependa kuyaweka wazi ila ninachotaka mashabiki wangu wakijue nipo salama kabisa,”

Jana Kamanda wa Kanda ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema rapper huyo juzi alihojiwa kituoni hapo na yupo nje kwa dhamana, huku jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tuhuma zinazomkabili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents