Burudani

Nay wa Mitego kuachia video ya wimbo ‘Wapo’ muda wowote

Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego amewataka mashabiki wake wa muziki kukaa mkao wa kula kwajili ya ujio wa video yake mpya ya wimbo ‘Wapo’ ambao unafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.

Rapa huyo aliiambia Bongo5 kuwa kabla ya kufanya remix ya wimbo wake huo kama alivyoagizwa na Rais Magufuli, ataachia kwanza video ya wimbo huo.

“Nakukabidhi sindano ya kulidunga, daktari haogopi ukubwa wa kidonda, we si doctor wa majipuu tumbua hakuna kuvunga.. #Wapo Video kesho iko tayari. Subscribe kwenye YouTube Channel yangu sasa #MrNay,” Nay wa Mitego aliandika Instagram.

Awali wimbo huo ulifungiwa na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kwa kigezo cha maadili na baadae Rais Magufuli kutaka wimbo huyo upigwe kwa madai hauna tatizo kama baadhi ya taasisi nyingine za serikali zilivyodai.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents