Habari

Nchi 70 zaitaka Korea Kaskazini kuwachana na nyuklia, saini ya Urusi na China zakosekana

Jumla ya nchi 70 zimeitaka Korea Kaskazini kuachana na mipango yake wa silaha za nyuklia, makombora ya masafa marefu na mipango mingine inayohusiana na shughuli hizo, zikilalamikia kitisho kisichokuwa na kikomo kwa amani ya dunia.

North Korea fired two short-range missiles on Thursday and carried out a drill last Saturday

Kwa mujibu wa shirika la habari la nchini Ujerum,ani, Deutsche Welle Nchi zilizotia saini tamko hilo ni pamoja na Marekani, Korea Kusini, Singapore na mataifa ya Asia, Amerika ya Kusini, Afrika na Ulaya.

Urusi na China ambazo zinaiunga mkono Korea Kaskazini, hazikusaini waraka huo ulioandikwa na Ufaransa.

Waraka huo unaitaka Korea Kaskazini kuepusha uchokozi wa aina yoyote, na kuendelea na mazungumzo na Marekani kuhusu makubaliano ya kuwachana na silaha za nyuklia.

Nchi hiyo ilifyatua makombora mawili ya masafa marefu siku ya Alhamisi kufuatia mazoezi ya awali siku ya Jumamosi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents