Habari

Nchi hii ni tajiri – Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa nchi ya Tanzania ni tajiri sana ila tumeshindwa kusimamia rasilimali zetu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli

Rais Magufuli amesema kuwa Tanzania ndiyo nchi pekee iliyobarikiwa na mwenyezi Mungu kuwa na madini ya Tanzanite duniani, lakini madini hayo bado hayatusaidii kwa chochote kwani matatizo bado yapo pale pale.

Kuna changamoto nyingi zinazolikabili taifa letu, Changamoto zipo zingine ambazo tumezidekeza sisi wenyewe, ni kwa sababu tumeshindwa kusimamia rasilimali zetu, nchi hii ni tajiri, na nyinyi ndugu zangu wa Simanjiro ni mashahidi, kwamba nchi hii ni tajiri, historia ya dunia hii inazungumza wazi kwamba wananchi wa Simbanjiro na Tanzania tulipendelewa na mwenyezi Mungu tukapewa madini ambayo hayapo mahali kokote kwenye dunia hii. Nenda Marekani, nenda Uingereza, nenda Urusi, nenda China, hakuna madini yanayoitwa Tanzanite yanachimbwa, yanachimbwa hapa Mererani, lakini tujiulize sisi wote Watanzania na Wanamererani haya madini yanatusaidia sisi? Mungu ametupa madini lakini sisi tunapata shida.“amesema Rais Magufuli leo asubuhi wakati akihutubia wakazi wa Simanjiro.

Rais Magufuli leo jumatano ameanza ziara yake mkoani Arusha ambapo amefungua barabara ya Lami kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) hadi Mererani wilayani Simanjiro.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents