Habari

Nchi hii yaindoa Nigeria kama mzalishaji mkuu wa mafuta Afrika

Nigeria imetolewa kwenye kiti chake kama mzalishaji mkubwa wa mafuta barani Afrika.

nigeria operations worker_inline full

Uzalishaji wa mafuta nchini Nigeria kwa sasa upo chini ya Angola baada ya mashambulizi mbalimbali kwenye miundombinu yake na kundi jipya la waasi, Niger Delta Avengers, kwa mujibu wa BBC.

Utafiti uliofanyika mapema mwezi huu umeonesha kuwa uzalishaji wa mafuta wa Angola ulikuwa mapipa milioni 1.8 kwa siku mwezi April huku Nigeria ukiwa mapipa milioni 1.69.

Na sasa Reuters Africa imeripoti kuwa Nigeria inazalisha mapipa milioni 1.4 kwa siku.

Kundi la Avengers linataka wakazi wa eneo la Niger Delta kuwa na umiliki wa mafuta, na maisha bora.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents