Habari

Nchi yetu imefungua ukurasa mpya – Mhe. Zitto

Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa nchi imefungua ukurasa mpya baada ya kutokea tukio la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kupigwa risasi eneo la tumboni na mkononi na watu wasiojulikana akiwa Mkoani Dodoma.

Zitto ameanisha hayo kupitia ukurasa wake wa facebook mara baada ya kutokea taarifa ya kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na watu wasiyofahamika ambapo Jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi.

Mbunge mwenzetu wa Singida Mashariki amepigwa risasi nyingi na watu wasiojulikana. Kakimbizwa hospitali Dodoma.
Nchi yetu imefungua ukurasa mpya. Wananchi tusimame imara tusikubali Kabisa kuingia kwenye siasa za namna Hii. Mola amponye ndugu yetu
ameandika Zitto.

Jeshi la polisi Mkoa wa Dodoma limelaani tukio hilo na uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents