Nchimbi aingia kandarasi ya miaka miwili na Azam FC

Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Majimaji na Mbeya City, Ditram Nchimbi ameingia kandarasi ya miaka miwli na Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC ikiwa ni maandalizi ya kuelekea msimu ujao.


Kutua kwa Nchimbi ndani ya Azam FC ni sehemu ya kuhakikisha klabu hiyo iliyo maliza ligi kwa kushika nafasi ya pili inafanya vema msimu ujao na mashindano mbalimbali.

Usajili huo unaifanya Azam inafikisha jumla ya wachezaji watatu waliyo ingia kandarasi kuelekea msimu ujao baada ya kutangulia nyota wawili kutoka Zimbabwe mshambuliaji Donald Ngoma na kiungo Tafadzwa Kutinyu, wote wakipendekezwa na Kocha Mkuu mpya, Hans Van Der Pluijm.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW