Habari

Ndalichako azindua maabara ya Hisabati Dar

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amezindua maabara ya somo la Hisabati iliyopewa kwa jina la ‘Hey Mathematics Programme’ na kusema itawezesha wanafunzi kufurahia na kuona urahisi wa kusoma somo hilo.

Akizindua maabara hiyo jijini Dar es Salaam, Waziri huyo amesema mpango huo utasaidia kujenga msingi mzuri wa somo la Hisabati kwa wanafunzi.

“Kama tunavyojua watoto wetu wanapenda mambo ya teknolojia, unakuta mara nyingi wako kwenye simu wako kwenye komputa kwahiyo ni mfumo ambao unaendana na vitu ambavyo vinawavutia vijana. Ni dhahiri kwamba kama una utiwa na kitu uwezekano wa kukifanya vizuri ni mkubwa kuliko jambo ambalo halikuvutii,’ alisema Ndalichako.

BY: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents