Habari

Ndege ghali zaidi ya kivita F35B ya Marekani yapata ajali, hii ni kwamara ya kwanza kuwahi kutokea

Ndege ghali zaidi ya kivita aina ya F35B ya taifa la Marekani imeripotiwa kupata ajali hapo juzi siku ya Alhamisi hii ikiwa ni kwa mara ya kwanza kuwahi kutokea kwa tukio kama hilo.

Ndege ghali zaidi ya kivita aina ya F35B ya taifa la Marekani

Vyomba mbalimbali vya habari vimeeleza kuwa ndege hiyo inayogharimu takriban dola milioni 100 za Marekani ndio ghali zaidi ya kivita kuwahi kutengezwa.

Kwa mujibu wa msemaji wa Marine Corps Capt. Christopher Harrison amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo aina ya F35 huku dereva ‘pilot’ akiwa salama na hakutokuwa na mejeruhi.

Ndege hii inauwezo wa kukwepa kutambuliwa na mitambo ya radar mbali na kuwa na uwezo wa kufyatua makombora upande wowote. Uchunguzi wa nini kilisababisha ajali hii ya F35B umeaanza, Ndege iliundwa na kampuni ya Lockheed Martin.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents