Tupo Nawe

Ndege iliyotengenezwa na wanafunzi wa Afrika Kusini, yatumia muda wa wiki 6 kufika Cairo Misri, waeleza walivyopata misukosuko wakiwa angani kwa kuanza kuvujisha mafuta

Ndege iliyotengenezwa na wanafunzi wa Afrika Kusini imetua salama Cairo, Misri wiki sita baada ya kuondoka Cape Town, Afrika Kusini. Ndege hiyo yenye viti vinne aina ya Sling 4 plane ilitengenezwa na kundi la wanafunzi 20 kutoka familia tofauti. Jumla ya wanafunzi sita walishiriki katika safari hiyo kama marubani na watoa msaada wa kiufundi.

Kwa mujoibu wa BBC. Safari yao ya kilomita 12,000 ilikuwa na vituo nchini Namibia, Malawi, Tanzania (Zanzibar na Kilimanjaro), Uganda na Ethiopia.

Rubani Megan Werner, msichana wa miaka 17, aliyeanzisha mradi wa U-Dream Global ambao ndio umewezesha safari hiyo amesema amefurahia mno mafanikio yao.

“Nimefarijika sana kwa hiki tulichokifanya, tumeonesha utofauti ndani ya bara (Afrika) katika sehemu zote tuliposimama.

“Lengo la mradi ni kuonesha Waafrika kuwa kila kitu kinawezekana kama utaweka akili yako katika kulifanikisha hilo,” amesema.

U-Dream Global project team
Image captionHuree!

Wanafunzi hao walikuwa wakitoa mihadhara kwa wanafunzi wenzao kwenye kila nchi waliyosimama.

Ndege nyengine aina ya Sling 4, ilikuwa ikiambatana nao na kuendeshwa na marubani wenye uzoefu ili kutoa msaada pale unapohitajika.

Baba wa Megan, Bwana Des Werner ambaye ni rubani mwandamizi alikuwa ni sehemu ya timu ya msaada.

Wanafunzi hao waliitengeneza ndege hiyo kwa wiki tatu kwa kuunganisha vifaa vilivyotengenezwa na kampuni moja nchini humo. Uundaji huo ulihusisha kuunganisha maelfu ya vifaa vidogo vidogo.

Hata hivyo, mafanikio hayo hayakukusa changamoto, ameeleza Megan.

Wanafunzi hao walikataliwa na mamlaka za Kenya kutua jijini Nairobi na ikabidi wabadili njia.

Katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, walichelewa kupata mafuta.

“Baada ya kuyapata, ndege ya pili ya msaada ikaanza kuvujisha mafuta na ikashindwa kuendelea na safari nasi na ikabaki marubani wawili tu mimi na Driaan van den Heever kuendelea na safari,” ameeleza Megan.

“Tulikuwa na mashaka juu ya kupaa katika anga la Sudani kutokana machafuko ya kisiasa yanayoendelea.”

Teenagers assembling the Sling 4 plane in South Africa
Image captionNdege hiyo iliundwa na wanafunzi 20 kutoka familia tofauti Afrika Kusini

Marubani hao sita wanafunzi walikuwa wakipokezana kurusha ndege hiyo.

Hata hivyo, aina ya leseni waliyopata ambayo ni daraja la kwanza pia ikawa kikwazo. Walitakiwa kutopaa juu sana na kufikia usawa wa mawingu.

Kipande cha mwisho cha safari kilikuwa ni mtihani mgumu kwa marubani hao.

“Tuliendesha ndege na Driaan van den Heever kwa saa 10 bila ya ndege ya usaidizi, ilikuwa ni wanafunzi wawili angai bila usaidzi wowote,” ameeleza Megan.

U-Dream Global project team
Image captionMarubani wanafunzi (kutoka kkushoto) van den Heever, Werner na Hendrik Coetzer
Presentational white space

Marubani hao wawili wanafunzi wakapatwa na tatizo katika mifumo ya ndege hiyo muda mfupi baada ya kuingia kwenye anga la Misri. Hivyo wakafanya maamuzi ya kutua kwenye uwanja wa karibu zaidi badala ya ule wa Kimataifa wa Cairo kama ilivyokuwa imepangwa awali.

“Halai hiyo ilizua tafrani kidogo, lakini maamuzi yalifanyika kwa sababu za kiusalama,” ameeleza Des Werner.

Ramani

“Mwishowe tukagundua kuwa ilikuwa nyanya moja tu imecheza na wakairekebisha mara moja, lakini kukawa na urasimu mkubwa ambao ulichukua muda mrefu na kutakiwa na mamlaka waandike ripoti.”

“Tulipotua Misri kwa dharura katika eneo la kwanza maafisa walitaka kutukamata, kutupokonya hati zetu za kusafiria na leseni lakini kwa bahati nzuri baada ya saa kama nne kila kitu kikawa sawa tukapata mafuta ya ziada ya kutufikisha Aswan, na kutoka hapo tukapaa mpaka hapa Cairo, lilikuwa ni jambo la furaha sana kutua Cairo,” ameeleza Megan.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW